NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Friday, April 12, 2013

Tanzania yapanda katika viwango vya ubora wa soka duniani kutokea nafasi ya 119 hadi 116.


Ushindi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliopata katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco umeisaidia kuipandisha nchi katika viwango vya ubora wa soka duniani.

Katika orodha hizo za kila mwezi zilizotolewa leo Tanzania imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 119 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 116 hivyo kuendelea kufanya vyema ukilinganisha na mwaka jana.

Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania wameendelea kung’ang’ania kileleni mwa orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina katika nafasi ya tatu huku kwenye nafasi ya nne kukiwa na ingizo jipya la nchi ya Croatia waliopanda wa nafasi tano mpaka kufikia ya nne na tano bora inafungwa na Ureno.

Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast wameendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kupanda kwa nafasi moja duniani mpaka nafasi ya 12 wakifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili ambao wao wamedondoka kwa nafasi mbili mpaka ya 22 duniani.

0 maoni: