NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Thursday, March 28, 2013

MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEKUFA CHUMBANI


Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa na jeraha lolote. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katikachumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert. 
 
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwa mwaka wa pili. 
 
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM. 
 
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala na wanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili ya masomo.
 
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuo hiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi. 

0 maoni: