NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Thursday, March 14, 2013

Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa zaidi ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vyumba 24 vya madarasa'
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa zaidi ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vyumba 24 vya madarasa katika shule ya Sekondari Nzondahaki iliyopo kata ya Nzovwe.Akiongea na Mwandishi wa habari hii Afisa mtendaji wa kata hiyo Furaha Malele amesema fedha hiyo itasaidia kukamilisha vyumba vya madarasa 24 kati ya vyumba 32 vilivyopo kwenye shule hiyo.Amesema fedha hizo zitatumika katika kununua saruji kwa ajili ya sakafu na ripu, mbao za kenchi, mabati ikiwa ni pamoja na kugharamia kupaka chokaa kwenye vyumba vyote 24.Wakati huohuo ameahidi kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo ndani ya siku 7 ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao katika hali nzuri.

0 maoni: