NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Thursday, June 21, 2012

WATOTO WA KIKE WAMEKUWA WAKIKOSA HAKI YA MSINGI YA KIELIMU KUTOKANA NA KUOZESHWA.

Na mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa haki za binadamu mkoa wa Mbeya Said Mohammed amesema watoto wa kike waishio wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,wamekuwa wakikosa haki ya msingi ya kielimu kutokana na wazazi kuwaozesha watoto wao wakiwa wadogo.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii,ofisini kwake na kuongeza kuwa ndoa za utotoni zimekuwa chanzo kikubwa kwa watoto kushindwa kuendelea na masomo.

Aidha amesema pamoja na Serikali kuwa na mkakati wa kuwawezesha watoto wa kike kielimu jitihada hizo zimekuwa zikishindikana kutokana na ndoa za utotoni na wazazi kuwaficha watu wanaohusika kuwapatia ujauzito watoto wao.

Kuhusu hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali Bwana Mohammed amesema inakuwa ni vigumu kuzitambua kutokana na mchakato wa kesi hiyo kuwa mgumu kwa sababu ya wazazi kushindwa kutoa ushahidi mahakamani.

0 maoni: