NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Wednesday, January 11, 2012

MWALIMU AIBIWA PIKIPIKI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 1.6 - MBOZI, MBEYA

Habari na Mwandishi wetu.
Watu wasofahamika walichimba ukuta wa nyumba ya Mwali Benard Wazingwa Mgala  ambaye ni Mwalimu wa Shule ya msingi Zelezeta Kata ya Igamba na kuiba pikipiki aina ya Skyeagle yenye nambari T 787 DAY rangi nyeupe na nyekundu,  yenye thamani ya shilingi milioni 1,600,000 za kitanzania iliyonunuliwa miaka miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Mwalimu Benard amesema kuwa pikipiki hiyo imeibiwa majira ya saa 10:00 alfajirii kwani mkewe alitoka nje majira ya saa 9 usiku pikipiki hiyo ilikuwepo.

Tukio hilo limeripotiwa Kituo cha Polisi Mlowo, wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote na jeshi lake linafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na matukio yote.

0 maoni: