NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Tuesday, December 13, 2011

NG'OMBE 6 WALIOIBIWA WILAYANI MBARALI WAKUTWA WILAYANI CHUNYA - MBEYA

 Ng'ombe waliochukuliwa na Jeshi la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi  Makongorosi wilayani Chunya wakiwemo ng'ombe 6 walioibiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
 *****
Habari ba Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Ng'ombe 6 walioibiwa Desemba 2, mwaka huu katika kijiji cha Mahango Kata ya Ruiwa wilayani Mbarali wamepatikana Desemba 10, mwaka huu katika kijiji cha Mkola, Kata ya Makongorosi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ambapo mifugo hiyo ni mali ya mfugaji Bwana Mensa Dick Mbembela.

Mifugo hiyo ilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi milioni 5.2 ilikamatwa katika kijiji hicho ikiwa na mifugo mingine ambapo mmiliki wa mifugo hiyo alikimbia na Jeshi la polisi kuichukua mifugo hiyo mpaka kituo cha polisi cha Makongorosi na utafiti ukifanyika ili kuweza kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kuwakamata waliohusika na tukio la wizi wa mifugo hiyo.

0 maoni: