NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Friday, October 7, 2011

MWANANCHI AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI OLD VWAWA + MBOZI MKOANI MBEYA

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
*****
Na mwandishi wetu
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametamka kwamba wananchi wenye hasira kali wamempiga kisha kumchoma moto Godi Adamu mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa old Vwawa wilayani Mbozi wakimtuhumu kuhusika na wizi.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda Nyombi amesema wanachi walifikia hatua hiyo baada ya kumkuta marehemu Godi akijaribu kuvunja nyumba ya Damson Kapushi mwenye umri wa miaka 56 mkazi wa Sogea Tunduma.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linamshikilia bwana Kapushi kwa mahojiano zaidi.

Wakati huohuo amewataka wananchi kutojichukulia sheria mkoani pindi wanapomkamata mwizi na badala yake amewataka wamfikishe katika vyombo vya sheria ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.

0 maoni: