NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Tuesday, October 11, 2011

KUPASUKA KWA KEBO YA KUSAMBAZIA UMEME, SAI JIJINI MBEYA NDIO CHANZO CHA MKOA KUWAGIZA.


Na mwandishi wetu
Imeelezwa kwamba tatizo la umeme linaloyakabili baadhi ya maeneo mkoani Mbeya kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa kebo inayosambaza umeme kutoka Sai eneo la mwakibete kwenda Iyunga.

Akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake meneja wa TANESCO Injinia Kyando amesema kuwa tatizo hilo limeshapatiwa ufumbuzi na hadi sasa wanaendelea na marekebisho eneo la Iyunga na kwamba mpaka kufikia  jioni ya leo zoezi hilo litakuwa limekamilika.

Ameongeza kuwa kutokana na matengenezo yanayoendelea umeme utakatwa siku nzima ili kuepukana na hatari ambayo inaweza kutokea kwa wananchi na kusababisha athari.

Aidha amewaomba radhi wananchi mkoani hapa kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na marekebisho hayo.

0 maoni: