NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Sunday, September 11, 2011

ZAWADI NONO YA SHILINGI LAKI TANO KUTOLEWA NA MAMLAKA YA MAJI MBEYA KWA MTU ATAKAYE FANIKISHA KUPATIKANA KWA WEZI WA GATE VALVE.

Mamlaka ya maji safi na maji taka jiji la Mbeya imetangaza kutoa zawadi ya shilingi laki tano kwa mtu atakaye toa taarifa ama kufanikisha kupatikana kwa wezi wa vifaa vya kuungia mabomba.

Akiongea na chanzo chetu cha habari cha kuaminika, Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo jijini hapa Injinia SHAURI amesema zawadi hiyo itatolewa ili kudhibiti vitendo vya wizi wa viungio vya mabomba katika mabomba mapya.

Amevitaja vifaa mbavyo vimekuwa vikiibiwa kuwa ni Gate valves zenye kipenyo milimita 75 hadi 400 na kuongeza kuwa mamlaka hiyo itaichukuwa taarifa iliyotolewa kuwa siri kubwa.

0 maoni: