NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Thursday, September 29, 2011

TIBA YA KIKOMBE CHA JAFARI MKOANI MBEYA YASIMAMISHWA KUTOKANA NA SABABU MAALUMU HAZIRUHUSU KUENDELEA KUTOLEWA.


 Na mwandishi wetu.
Kijana Fikiri Jafary mwenye umri wa miaka 17 mkoani mbeya eneo la mabatini amesitisha zoezi la utoaji wa kikombe kwa sababu maalumu ambazo hazimruhusu yeye kuendelea na zoezi hilo la utoaji dawa.

Mratibu wa tiba za asili mkoani hapa Bwana Boniventure Mwalongo amesema kuwa kijana huyo aliyekuwa akitoa huduma ya kikombe amekatazwa kutoa huduma hiyo kwasababu hajakidhi vigezo na masharti katika utoaji wa huduma ya tiba ya asili.

Aidha ameongea kuwa kijana huyo alikuwa hajafuata taratibu za kujisajili kama mganga wa tiba za jadi na umri wake hauruhusu kuwa mtaalamu wa tiba za asili kwa kuwa hakufikisha umri wa miaka 18 na hakuwa mtaalamu miaka ya nyuma kabla ya kuanzisha kikombe.

0 maoni: