NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Friday, September 16, 2011

MRADI WA JOSHO ULIOGHARIMU MILIONI 24 KIJIJI CHA LUHANGA MBARALI MKOANI MBEYA WAFUNGULIWA TAYARI KWA MATUMIZI

Na mwandishi wetu.
Zaidi ya shilingi milioni 24 zimetumika katika ujenzi wa josho la Ng'ombe lililopo kijiji cha Luhanga wilayani Mbarali, ambapo kukamilika kwa josho hilo ni kuwasaidia wafugaji kuwakinga ng'ombe wao dhidi ya magonjwa.

Akizindua josho hilo, Mganga mkuu msaidizi wa mifugo wa wilaya ya Mbarali Dakta Tuliano Nswira ametoa pongezi kwa kamati ya ujenzi wa josho kutokana na uaminifu waliouonesha wa kutunza fedha zilizochangwa na wafugaji.

Naye, Afisa mtendaji wa kijiji cha Luhanga Bwana Khamis Mlamata amesema mafanikio ya ujenzi huo yametokana na ushirikiano bora uliopo kati ya viongozi wa kijiji na wananchi wa kijiji hicho.

Kamati ya ujenzi iliyosimamiwa na Bwana Saidi Nyang'ondo ambaye ni mwenyekiti, katibu wake Bwana Charles Juma ambao wote kwa pamoja wamesema kuwa siri ya mafanikio yao ni ushirikiano na uwazi katika utendaji kazi.

0 maoni: