NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Tuesday, September 13, 2011

MAISHA MAGUMU MTINDO MMOJA MBEYA KAMA MWISHO WA DUNIA USIVYOFAHAMIKA.

Na mwandishi wetu.
Mtoto Yusufu Kyando mwenye umri wa miaka 9 amesema analazimika kuwa ombaomba na kuokota chupa za maji kwenye ghuba za taka kwa ajili ya kwenda kuziuza ili apate fedha zitakazomwezesha kujikamilishia mahitaji yake muhimu.

Amesema kuwa alianza kukosa huduma muhimu kutoka kwa wazazi wake baada ya wazazi hao kutengana na kuongeza kuwa bado ana moyo wa kujiendeleza kimasomo endapo atapata mfadhili wa kimuendeleza kielimu.

Nao baadhi ya wakazi wa kata ya Uyole wametoa ushauri kwa wazazi kutoa huduma kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kuondoa chuki kwa watoto endapo wao watakabiliwa na migogoro ya kifamilia.

Mmoja wa wakazi hao bwana Abas Othman amesema wamekuwa wakizurula mitaani kutokana na kukosa mahitaji muhimu kama mavazi na chakula.

0 maoni: