NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Saturday, August 20, 2011

WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI MBEYA WAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA VITENDEA KAZI

 Shughuli zikiendelea katika mgodi wa Chunya.
Wachimbaji wadogowadogo wa madini mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwawezesha vifaa vya uchimbaji wa madini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Ombi hilo limetolewa na mmoja wa wachimbaji hao Bwana Daniel Mwaisabila wakati wa mahojiano kuhusu namna ambavyo Serikali ingeliweza kuwasaidia katika shughuli zao za madini.

Amevitaja vifaa wanavyotumia kwa ajili ya shughuli hizo za uchimbaji wa madini kuwa ni Sululu na koreo ambavyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha ufanisi wao wa kazi

Hata hivyo amewataka vijana kujituma katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili waweze kujikwamua dhidi ya umasikini.

0 maoni: