NEW VIDEO:- CHRIS BEE - BASHEE

https://2.bp.blogspot.com/-NZDdQwpgbRw/WMA34hEugXI/AAAAAAAATag/4I0Huz3ca6kOQZL8h9gKQy7MN1039AuYwCLcB/s1600/sdfghjk.png

Pages

Thursday, August 25, 2011

UFAYATUAJI WA TOFARI WASABABISHA MAHUDHURIO KUWA HAFIFU KATIKA SHULE YA SEKONDARI REJIKO.

Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Rejiko iliyopo kata ya Majengo jijini Mbeya wamekuwa wakishindwa kuhudhuria vipindi darasani kutokana na kutumikia adhabu ya kufyatua matofali.

Wakiongea na Bomba Fm wanafunzi wa shule hiyo wamesema licha ya adhabu ya kufyatua matofali 200 kwa kila mwanafunzi pia wamekuwa wakipewa adhabu ya viboko sita na kuchaniwa sare za shule.

Kutokana na adhabu hizo wanazokabiliana nazo wameiomba Serikali kuingilia kati adhabu wanazokabiliana nazo kwani zimekuwa zikiwasababishia baadhi yao kuvaa sare zilizochanika ikiwa ni pamoja na kushindwa kumudu vyema masomo yao kutokana na muda mwingi kuutumia kwa ajili ya kufyatua matofali.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joshua Mwakitalima amesema adhabu hizo zinatolewa kwa wanafunzi watukutu na kuongeza kuwa baadhi yao wamekuwa wakinyang’anywa viatu.

Jitihada za Bomba Fm kuwasialiana na afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda zimeshindikana baada kiongozi huyo kuwa mkutanoni.

0 maoni: