Social Icons

.

Pages

Featured Posts

.

Monday, February 27, 2017

LADY JAYDEE AKIICHAMBUA ALBAMU YAKE YA WOMAN NA ATANGAZA KUTOKA MACHI 31, 2017Super Woman LADY JAYDEE aitaja rasmi tarehe 31/3/2017 kuwa ndio wakati maalumu wa kuiachia albamu yake ya Saba iitwayo WOMAN, inayotoka chini ya Record Label ya ROCKSTAR 4000.


Hitmaker huyo wa Sawa na Wao ni miongoni mwa wasanii wakongwe wenye mafanikio makubwa katika music industry katika kuutangza muziki wa Bongo Flava kimataifa, pia ni kivutio cha mabinti wengi walioingia katika tasnia ya muziki kwa kufuata nyayo zake.

Kupitia Kipindi cha The Splay ya Ebony FM Redio, amezungumzia tofauti ya Albamu ya Binti na Woman, wasanii walioshirikisha na njia atakazotumia kuiuza alamu hiyo.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA LADY JAYDEE


Albamu zake nyingine zilizowahi kufanya vema ni pamoja na Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), "Nothing But The Truth (2013).

Niliposhuka kimuziki na kimaisha kuna watu walininyanyasa hadi kutaka kunikwapua mke – Hussein Machozi

Kwa msanii au mtu maarufu, kinga pekee inayomsaidia kuendelea kuwa na heshima yake, ni kuwa na wimbo unaofanya vizuri ama kuwa na fedha.

Anapokosa hivyo, mambo hubadilika na hapo ndipo ule usemi wa Fid Q kuwa usupastaa ni mzigo wa miiba huwa na maana. Hussein Machozi anaijua hali hiyo na kupitia mitihani aliyopitia miaka miwili iliyopita, amejifunza mengi.

“Nimejifunza kuna watu wa kweli na kuna watu feki,” Machozi ameiambia Bongo5.

“Kuna watu wa kweli ambao wamekaa na mimi kwa shida mpaka sasa hivi wapo na mimi, marafiki wa kweli. Na kuna watu baadhi ambao walikuwa wapo karibu sana na mimi kipindi nipo juu, lakini kipindi ambacho nilikuwa kimya kwa muda mrefu, wameniacha mbali wamenitupa,” anasema.

“Wamenisahau,wameninyanyasa, imefikia kipindi wengine wanatongoza mpaka mke wangu. Ni kitu ambacho kinauma sana na sio kwamba mtu anamtongoza mtu hamjui, anamtongoza anajua kabisa huyu ndio future ya Hussein Machozi, yaani ndio mtu anayemtegemea. Siwasemi wengine ni mabosi walikuwa wanajifanya mabosi na vitu kama hivyo. Lakini yote tupilia mbali, ni kwamba mimi nasonga mbele na maisha naendelea na maisha yangu, nimesahau mabaya yote, nimefungua ukurasa mpya.”

Machozi ambaye kwa sasa anaishi nchini Italia amesema amenyanyuka tena na sasa yupo tayari kurudi kwenye muziki. Anatarajia kuachia kazi yake mpya iitwayo Nipe Sikuachi.

Thursday, February 23, 2017

WALIOTAKA KUMWABUDU KANYE WEST WAPEWA SANAMU YAKE….

 


Mtengeneza sanamu maarufu mjini Las Angels ‘Ginger’ ametengeneza sanamu ya Kanye West iliyofananisha na picha ya Yesu Kristo.

Msanii huyu aliyetengeneza sanamu hi anasema sababu za kutengeneza na kuiweka wazi kwa watu ni kama njia ya kuonyesha matatizo aliyopitia Kanye West mwaka 2016 kuelekea mwaka 2017 kama Kulazwa hospitalini kwa matatizo ya akili, kumpa ushirikiano rais Donald Trump na kupondwa vikali na watu weusi kwa kukutana na Donald Trump.

Sanamu hii ni ya Plastic na mtengenezaji huyu anasema sababu zingine ni “Kutoa sifa kwa Kanye West kana Producer na mwandishi bora wa muziki ila watu wajue yeye sio Mungu na mpaka alipopata matatizo ndipo kila mtu akaanza kumtukana na kumkejeli, ni sawa na kama walimuweka kwenye msalaba, mambo kama haya tumeyaona yakifanyika kwa wasanii kama Britney Spears na Lindsay Lohan, watu hao hao wanaomuona yeyeni kama Mungu wao ndio baadae wanamtesa“.

 

Polisi amuua mwenzake kwa kumpiga risasi na yeye ajiua baada ya mechi.

Polisi huko nchini Kenya, amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na yeye amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya Manchester City na Monaco.

Kabla ya polisi huyo, Konstebo Constable Patrick Kihagi kujiua kwa kujipiga risasi kichwani, alimjeruhi polisi mwingine kwa kumpiga risasi begani.

Polisi aliyekufa ametajwa kwa jina la Konstebo James Makokha, na kabla ya kifo alikuwa akifanya kazi Jogoo House. Inadaiwa kuwa Makokha alipigwa risasi wakati akitaka kumaliza ubishani kati ya Kihagi na Ng’etich.

Kabla ya tukio hilo saa saba na nusu usiku kwenye eneo la Tassia, Nairobi nchini Kenya, polisi hao watatu walikuwa baa wakitazama mpira na kisha wakaanza kubishana, wakatoka nje.

 Mashuhuda wanadai kuwa, walipotoka nje walizidi kubishana, Kihagi akatoa bastola na kumjeruhi mwenzake, Konstebo Dominic Ng’etich kwa risasi.

Kihagi alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Embakasi, Ng’etich anafanya kazi kwenye kituo cha polisi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

By: Emmy Mwaipopo
Chanzo: Habarileo

Tuesday, February 21, 2017

HUSSEIN MACHOZI KUVUNJA UKIMYA NA ‘NIPE SIKUACHI’ CHINI YA COMBINATION SOUND

Dar es Salaam, Tanzania, February 21, 2017

Baada ya kukaa kimya kwa miezi mingi bila kuachia wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia wimbo mpya wiki chache zijazo. Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Nipe Sikuachi.’

Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake za Combination Sound.

“Combination yangu ya mimi na Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” anasema Machozi ambaye amethibitisha kuanza kufanya kazi rasmi kwa uangalizi wa label ya mtayarishaji huyo mashuhuri nchini Tanzania.

“Man Walter ni mshkaji kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona kabisa kwamba sisi tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika japo tuna makubaliano ya kusaini.

 Kwahiyo ni mimi tu nirudi Tanzania tuje tukae tusaini, lakini ukweli ni kwamba mimi nafanya kazi chini ya uongozi wa Kombinega,” amesema.

“Video pia imefanyika Italy, Gressoney Italy. Kuna mabadiliko makubwa ukiangalia location ambazo tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona Tanzania za magari na majumba,” amesisitiza muimbaji huyo.

Machozi ambaye anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’, ‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya kimaisha.

“Kama unavyojua, hakuna mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi kadhaa nilishawahi kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya ukosefu wa management.

Kwa sasa Hussein anaishi nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo haimaanishi kuwa ameupa kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya.

“Ilikuwa ni kozi fupi ambayo kwa sasa imeisha na nafanya shughuli za kawaida kujipatia riziki,” anaeleza.

Machozi anakikisha kuwa ujio wake mpya utakuwa wa tofauti.

“Kinachokuja kuonekana sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na nimejaribu kufanya hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu ambacho ni kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba  ni kipya, video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”

Anasema tarehe rasmi ya kutoka kwa video na wimbo itatangazwa hivi karibuni. 

KUFAHAMU ZAIDI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI MFUALITIE KWENYE MITANDAO  YA KIJAMII:

NEW VIDEO: Makomando – Saula

Saturday, February 18, 2017

Mkiwa na uhakika, msiogope kuwaanika vinara wa unga – Waziri MkuuWaziri mkuu amewataka viongozi kutowatangaza watuhumiwa wa dawa za kulevya bila ya kufanya uchunguzi lakini wasiogope kuwaanika wale wenye uhakika kuwa kweli ni wauzaji.

Ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya katika ofisi ya Waziri Mkuu Ijumaa hii. Alisema wakuu wa mikoa wana nafasi nzuri ya kushiriki katika vita hiyo kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu. 

Alisema, “Kuendelea na zoezi hili Watanzania wanataka kujua hii vita inaendaje, msisite baada kuwakamata, mmejiridhisha kuwatangaza hadharani iwe mfano kwa wengine wote ambao wanakusudia au wanaendelea kwa siri kutumia au kujihusisha kwenye jambo hili la uchunguzi ambao utakuwa unaendelea. 

Watendaji wa mamlaka kila mmoja kwa nafasi yake mnapaswa kufahamu kuwa mmeaminiwa hivo inabidi muwe waadilifu sana kwani mmekabidhiwa majukumu makubwa yanayohitaji uangalifu wa hali ya juu.”

Aidha waziri mkuu alisema serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria kiongozi yeyote atakayejihusisha na rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

By: Emmy Mwaipopo

KAULI HII TUNAWEZA KUTAFSIRI MOJA KWA MOJA KUWA BONGE LA NYAU NA BOB JUNIOR WANA BEEF?Kama utakuwa umefuatilia vizuri, utagundua ngoma kadhaa za Bonge La Nyau zilizotoka hivi karibuni hazijatengeneza na mkali wa mindundo Bongo Bob Junior ikiwemo ngoma ya Vice versa, Aza(Mtoto wa Kariakoo) na Tusiachane.


Ngoma hizo mbili kati ya hizo zimepikwa na Producer Amiga Tyger, yafaa kukumbuka kuwa Bonge La Nyau wakati akichupukia katika game ngoma kama Gusa Unase, Wengi Walaghai, Uvumilivu zilipikwa na Producer Bob Junior.

Pengine ukawa na swali nini kipo chini ya carpet, kupitia The Splash ya Redio Ebony FM, mtu mzima Bonge La Nyau ameweka wazi uhusiano wao kwa sasa.

“Ha ha ha ha haaaaaa(anacheka) hapana sifanyi kazi na Bob Junior, ha ha ha haaaaaa, eeeeh ni swahiba wangu lakini sifanyi nae kazi, ila ana kazi zake na mimi nina project zangu” amesema Bonge La Nyau.

Ameongeza pia “Hapana hapana sijakutana na athari yoyote, kwa sababu hata ukisikiliza miziki niliyokuwa nikifanya na Bob Junior kipindi hicho manyimbo ya kuchezeka chezeka, lakini sasa hivi nimeimba nyimbo za hisia, kwa hiyo nimezidi kuchukua base nimesababisha muziki wangu umekuwa na marriage kubwa naweza nikatoa wimbo ukakaa mwaka na zaidi mfano mzuri wa ngoma ya Aza (Mtoto wa kariakoo) imekaa mwaka lakini ikiipiga leo ni ngoma ambayo inaishi na itaendelea kuishi”.

DOWNLOAD MY TRACKS

 
 
Blogger Templates